KAMA ni mgeni, ukifika Manispaa ya Mtwara-Mikindani unaweza usiamini unapoona mandhari ambayo ni taswira halisi ya mji huo, uliopo Kusini Mashariki mwa Tanzania.
Ni mji unaosifika kwa kuwa na ramani bora ya mipango miji nchini, ndiyo makao makuu ya Mkoa wa Mtwara, umeundwa na Tarafa Mbili, Kata 15, Mitaa 85 na vijiji sita wenye wakazi 156,000 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2002.
Kutokana na kukosekana kwa taa ambazo zingependezesha mji, pia zingepunguza matukio ya uporaji, yanayofanywa na vibaka, kandokando ya barabara.
Wakati hali ya miundombinu ya barabara ikiendelea kuwanyima raha wakazi wa Mikindani hasa wa Mangowela, Chuno, Chipuputa na Kiyangu baada ya mvua kunyesha, pia ongezeko la watu ni changamoto kubwa katika utoaji wa
huduma za jamii.
Ongezeko la watu
Ongezeko la watu limekuja baada ya vyuo vingi kufunguliwa, kikiwamo Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), Chuo cha Utumishi wa Umma na Chuo cha Kilimo Naliendele, mbali ya vile vikongwe vya ualimu, utabibu na Veta.
Kupatikana kwa gesi, na utafiti wa mafuta unaoendelea mkoani Mtwara pia kumeongeza idadi ya wageni katika mji wa Mtwara wenye nyumba nyingi za zamani, mbali ya watu wanaopita katika mkoa huo kwenda nchini Msumbiji kwa shughuli za biashara na kazi nyingine.
Kuongezeka kwa kasi ya idadi ya watu na kuwapo kwa shughuli mbalimbali, kumesababisha mji huo kuwa kivutio kwa wageni na wenyeji.
Langu moja tu, mji mchafu, hata wageni wanaoingia wanakaribishwa na uchafu, Meya mji wako ni mchafu, hii ni aibu kwetu naomba mamlaka husika kuchukua hatua,” anasema Simbakalia.
Maisha yapanda kwa kasi
Mbali na kuwapo kwa ongezeko la watu maisha yamebadilika sasa, Mtwara unayoijua wewe siyo ile ya mwaka 2000 au mwaka 2005. Sasa bei bidhaa mbali mbali imepanda kwa kasi, vifaa vya ujenzi ni gharama kubwa saa kutokana na kukuwa kwa mji wa manispaa hiyo.
Kwa mfano vyumba vya kulala wageni mwaka 2006, kimoja kilikuwa ni Sh5,000 mpaka Sh10,000 kutokana na ubora, lakini sasa ni Sh20,000 mpaka Sh50,0000. Kiwanja cha kujenga nyumba kimoja mwaka 2006 ilikuwa Sh200,000 mpaka Sh500,000, lakini sasa ni Sh3 milioni mpaka Sh8 milioni.
Kwa upande wa nyumba, moja ilikuwa ikiuzwa Sh5 milioni mpaka Sh8 milioni mwaka 2006, sasa ni Sh10 milioni mpaka Sh25 milioni.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara- Mikindani, Margaret Nakainga anasema manispaa hiyo ni miongoni mwa manisapaa saba zinazotekeleza mradi wa miaka mitatu wa kuendeleza majiji.
Anataja miji mingine amabayo inatekeleza mradi huo kuwa ni Arusha, Mbeya, Kigoma, Mwanza, Dodoma Makao Makuu (CDA) na Dodoma Manispaa.
Wapewa Sh17 bilioni za kuendeleza Mtwara
Mradi huo ni wa miaka mitatu kuanzia 2010 mpaka 2012, umefadhiliwa na Benki ya Dunia (WB), hapa kwetu tumepata Sh17 bilioni ambazo zitatumika kujenga miundombinu ya mji, kuimarisha mifumo ya halmashauri katika kutoa huduma bora kwa jamii.
Zitajengwa barabara kwa kiwango cha lami zenye uwezo wa kuhimili uzito mkubwa, barabara hizi ni zile zinazoelekea bandarini na zingine za mitaani, lakini pia zitafungwa taa barabarani,anasema Nakainga.
Nakainga anasema awamu ya kwanza ya ujenzi wa barabara umehusisha barabara za Zambia yenye urefu wa kilomita 3.77 na bandari yenye urefu wa kilomita 2.75 ambazo zinajengwa upya kwa kiwango cha lami na kuweka taa za barabarani.
Anasema barabara ya Mtaa wa Mikindani yenye urefu wa kilomita 1.9 inajengwa kwa vitofali ili kutoleta athari kwa nyumba za asili katika mji huo mkongwe wa kihistoria.
Anabainisha kuwa ujenzi wa barabara hizo umeanza kupitia kampuni ya kizalendo ya Southern Link Ltd itakayotumia miezi 15 kukamilisha mradi huo kuanzia Oktoba Mosi, mwaka jana na kwamba manispaa yake imetumia Sh112 kulipa fidia kwa wakazi 52 ambao nyumba zao zimebomolewa kupisha mradi huo.
Katika awamu hii ya kwanza mradi huu wa ujenzi wa barabara umegharibu Sh12.7 bilioni, mchakato wa kuanza awamu ya pili ya mradi umeanza kwa kutafuta wazabuni, ni imani yangu kuwa kukamilika kwa mradi huu mji wa Mtwara utavutia,anaeleza mkurugenzi huyo.
Anasema awamu ya pili itahusisha barabara ya Kunambi yenye urefu wa kilomita 1.8 na Chuno yenye urefu wa kilomita 5.88 na kwamba awamu ya tatu, itahusisha ujenzi wa vizimba 25 na dampo la kisasa kubwa la hekta 7 katika eneo la Mangamba kwa ajili ya kuweka taka ili mji uwe safi.
Mkurugenzi huyo anasema katika kuimarisha mifumo ya taasisi, mafunzo mbalimbali yanatolewa katika idara za fedha, ujenzi, afya, mipango miji na upimaji ardhi,sanjari na ununuzi wa kompyuta, magari na vifaa vya kupima ardhi na ukarabati wa ofisi.
Nakainga anaeleza kuwa ofisi zilizokarabatiwa ni za mshauri mradi, mhandisi ujenzi, maendeleo ya jamii, masjala ya ardhi, uchumi na mipango.
Ofisa Habari wa manispaa hiyo, Jamadi Omari anasema jamii imepewa ya kujikinga na maambukizi mapya ya Visuri Vya Ukimwi (VVU) ili mradi huo usiache maafa.
Wafanyakazi wa mradi watakaa hapa kwa miezi 15, bila shaka watahitaji wanawake,unajaribu kuwakumbusha wasijisahau kupambana na ukimwi, wasiwaamini wafanyakazi katika mradi huo wakadhani ni salama,anasema Omari.
Tumewasisitizia kuepuka kufanya mapenzi, lakini ikiwa ni lazima, watumie kondomu, pia tumewapa elimu ya ujasiriamali, ili wafanye biashara ya mgahawa na zingine kwa lengo la kuwainua, kiuchumi,anasema.
Mstaiki Meya wa manispaa hiyo, Suleiman Mtalika anasema uamuzi wa manispaa yake kutoa zabuni kwa kampuni ya kizalendo unalenga kuongeza fursa kwa wazawa ili waitumikie nchi yao.
Suala kubwa ni uzalendo, kuweni wazalendo katika kusimamia mradi huu, mfano barabara ya Nangurukulu leo hii inajengwa upya kwa sababu kandarasi na wasimamizi walikosa uzalendo, hasa ninyi wahandisi washauri, hatutakubali kuona mambo yakienda ovyo.
Kuwapo kwenu hapa pia kuongeze fursa za ajira kwa vijana wetu, mradi wa Mtwara uanze kuwanufaisha watu wa Mtwara kwanza, tunao vijana wenye sifa na uwezo wa kufanya kazi hizo naomba wapewe kipaumbele,anasema Mtalika.
Vijana kupata ajira
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Southern Link Ltd, Mhandisi Joswam Mlaki anasema atatoa ajira kwa wakazi wa Mtwara.
Baadhi ya wananchi wanapongeza hatua hiyo ya Serikali na kuitaka kuwekeza nguvu kama hizo katika kutatua matatizo mengine ya kijamii kama kuanza miradi ya maji na elimu.
Tunasubiri kuona mwisho, unajua miradi mingi tatizo ni kutekelezwa chini ya kiwango, hali hiyo tutaibaini baada ya mradi kwisha, ila naipongeza Serikali kwa kuisukuma Mtwara, naomba nguvu kama hizo zielekezwe miradi ya maji na elimu, anasema Saleh Idd, makazi wa Chikongola.
Chanzo:
Habari na Abdallah Bakari, Mtwara
Gazeti la Mwananchi
12 Aprili 2012
No comments:
Post a Comment