KF Album

Hali ya baadhi ya nyumba za wananchi wetu kusini. Je, mtoto kutoka nyumba hii ataweza kupata elimu na malezi bora ili kuleta mabadiliko ya familia yake?
Viongozi wa Halmashauri ya kijiji cha Ikungu, Nachingwea wakijadiliana na viongozi wakuu wa SEDO (hawapo pichani) wakati wa ziara ya viongozi hao mikoa ya Lindi na Mtwara mwanzoni mwa mwaka 2007.
Hali duni ya upatikanaji wa maji ni tatizo mkoani Lindi kama picha inavyoonesha wakazi wa kijiji cha Somanga, Kilwa wakihangaikia maji. Wananchi hawa walielezea madhira yanayowakuta wakati wa kutafuta maji wakati walipokutana na uongozi wa SEDO mwanzoni mwa mwaka 2007 kijijini Somanga.
Katibu mkuu wa SEDO Bw. Omar Vumilia Sijale akikagua msingi wa majengo ya shule ya sekondari kwenye kijiji cha Naliendele, Mtwara wakati viongozi wakuu wa SEDO wakiwa ziarani mikoa yetu ya Lindi na Mtwara mwaka 2006.
Kumbukumbu: Mwenyekiti wa SEDO Bw. Geoffrey Katali Mwambe (kushoto) akiwa na mjumbe wa SEDO Mtwara Zuberi Mohamed (marehemu) katikati na mhasibu wa WABISOKO Mtwara (kulia) wakati kiongozi wa SEDO akiwa ziarani mikoa ya Lindi na Mtwara mwishoni mwa mwaka 2006. Marehemu Zuberi aliitumikia SEDO kwa utiifu mkubwa na hadi mauti yanamkuta miaka mitatu iliyopita alikuwa chachu ya ushiriki wa wafanyabiashara wa soko la Mtwara kwenye harakati za SEDO