Thursday, April 12, 2012

Tahadhari ya Tsunami Yafutwa ... Mikoa ya Kusini ni Salama

Ndugu wanakusini,

Tahadhari ambayo ilitolewa jana juu ya tishio la kutokea mafuriko ambayo yangesababishwa na tufani la Tsunami limeondolewa baada ya vipimo vya wataalamu kuonesha kuwa eneo la bahari ya Hindi kuelekea Afrika limesalimika. Kulingana na CNN na vyombo vinginevyo, kasi ya mawimbi ya Tsunami baharini imepungua sana na hivyo kuepusha mawimbi makubwa kufikia maeneo ya pwani za Afrika Mashariki.

Tunashukuru kwa mwitikio wa wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara kwa kuchukua tahadhari mapema. Pia tunatoa wito kwa wadau mbali mbali kutoa taarifa kwa SEDO na kupitia KF pindi tatizo lolote linapotokea au kutishia kutokea ili tuwapashe habari ndugu zetu na hivyo kuwaokoa na majanga.

Imetolewa na SEDO Sekretariati
Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment