Mafuriko yanayosababishwa na tufani la Tsunami lilioanzia huko visiwa vya Indonesia yanatarajiwa kugusa maeneo ya ukanda wa Bahari ya Hindi kupitia kisiwa cha Madagascar. Maeneo yanayohofiwa kuguswa na matokeo ya Tsunami hii ni pamoja na pwani za mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, DSM na Tanga. Matarajio ni kwamba pwani za Mtwara na Lindi zitaanza kupata matukio haya kuanzia saa 11.30 jioni ya leo tarehe 11 Aprili 2012.
Hivyo SEDO inatoa wito kwa wananchi wote wanaofanya shughuli zao baharini na kando kando ya fukwe za bahari kuchukua tahadhari kwa kuondoka maeneo hayo hatarishi. Pia SEDO inaomba Serikali mkoani Mtwara na Lindi kufanya mawasiliano na kufuatilia kwa kina taarifa zote ili kuwaandaa wananchi wetu wa kusini kujiepusha na janga la mafuriko.
Vyanzo mbali mbali vya Utabiri wa hali ya hewa na vyombo vya habari vimeripoti kuwa nchi zilizo kwenye hatari ya kukumbwa na Tsunami ingawa kwa viwango tofauti ni: INDONESIA, INDIA, SRI LANKA, AUSTRALIA, MYANMAR, THAILAND, MALDIVES, UNITED KINGDOM, MALAYSIA, MAURITIUS, REUNION , SEYCHELLES, PAKISTAN, SOMALIA,OMAN, MADAGASCAR, IRAN, UAE, YEMEN, COMORES, BANGLADESH, TANZANIA, MOZAMBIQUE, KENYA, CROZET ISLANDS, KERGUELEN ISLANDS, SOUTH AFRICA. (Soma: http://ptwc.weather.gov/ptwc/text.php?id=indian.TSUIOX.2012.04.11.0845).
Tutaendelea kuwapa taarifa kadri tunavyozipata. Ila mdau yeyote mwenye taarifa mpya asisite kuzituma kwa email: kusiniforum@gmail.com.
Imetolewa na SEDO Sekretariati
Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment