Ndugu Wanakusini,
Mnakaribishwa kwenye kikao chetu kitakachofanyika jijini DSM tarehe 15 April 2012 saa 8 mchana Mtoni Kijichi. Kikao hiki kitajadili maendeleo yetu wananchama na mafanikio na mikakati mipya ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi wetu wa Lindi na Mtwara mikoani kwetu.
Ukiwa mdau wa maendeleo ya kusini na kama ni mmoja wa wanaoguswa na pia kama una moyo wa kujitolea kwa maendeleo ya wengine basi unakaribishwa. Kila mmoja wetu ana haki ya kuwa mwanachama ilimradi ni mzaliwa, mwenyeji na ana mapenzi mema na kusini.
WITO: "Iwe ni fahari kuwa Mwanakusini, na guswa na maendeleo duni ya watu wetu"
Karibuni nyote na tuwaeleze wenzetu!
Imetolewa na:
Uongozi wa SEDO
Simu: 0784/0655 - 509891; 0784 503840; 0659 720072; 0784 804538
E-mail: kusiniforum@gmail.com
Blog: kusiniforum.blogspot.com
No comments:
Post a Comment