Friday, December 21, 2012

Salamu za Krismasi na Mwaka Mpya

Ndugu wanakusini, Taasisi yako ya maendeleo ya mikoa ya kusini ya Lindi na Mtwara (South Eastern Development Org - SEDO) inapenda kuwatakia kheri na afya kipindi cha sikukuu na kumaliza mwaka 2012. Pia tunawaombea wote tuvuke salama mwaka huu na kuuanza mwaka 2013 kwa Neema za Mwenyezi Mungu mwenyewe. SEDO inapenda kuwakumbusha slogan yake "Thamani ya mtu ni KUJENGA na KUENDELEZA kwao". Kwa hili tungependa tuanze mwaka 2013 kwa kila mmoja wetu kujichunguza ili kuona ana faida gani kwa jamii ya watu wake kule kusini, lipi umefanya la kuchangia maendeleo ya wasiojiweza, lipi unaweza kulifanya mwaka 2013 kuboresha au kuongeza juhudi kuliboresha na nini ambacho kipo mabegani mwako ambacho kina manufaa kwa wananchi maskini wa Lindi na Mtwara. Tukumbuke juhudi ya mtu mmoja mmoja ni muhimu ila ina tija ndogo kuliko kuunganisha nguvu. Hivyo, wanakusini mnaombwa mwaka 2013 tuutumie kujitazama na kuunganisha nguvu zetu ili kwa pamoja tushinde magumu yanayowakabili ndugu zetu na sisi wenyewe hasa kwenye matatizo ya Elimu, Afya, Soko la korosho na ufuta, mipango ya matumizi ya gesi asilia na migogoro ya ya viongozi ambayo haina tija kwa wananchi maskini. Imetolewa na Uongozi; South Eastern Development Organization - SEDO Ofisi ya Sekretarieti DAR ES SALAAM

2 comments:

  1. Kulikoni kimya wana SEDO? Naona majukum yamewabama tunawaaminia sasa ikiwa hivi?!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nakuunga mkono katika kuuliza hili swali. Kulikoni wana SEDO mbona kimya huku

      Delete