Monday, February 20, 2012

Juhudi Zafanywa Kukomboa Soko la Korosho Kusini

Viongozi mbali mbali wanafanya juhudi kubwa ili kukomboa soko la korosho lililoonekana kuyumba kwenye mikoa ya kusini ya Lindi na Mtwara. Mmoja wa viongozi hao ambaye ni Waziri amesema yeye, mawaziri wenzake na wakuu wa bodi ya korosho wanashughulikia suala hili wakishirikiana na wizara ya fedha. Lengo la juhudi hizi ni kuviwezesha vyama vya ushirika kuweka kununua korosho zote na ziwekwe maghalani.

Hata hivyo taarifa zitaendelea kutolewa hapa KF Jamii ili kuwakomboa wananchi wetu wa mikoa hii.

Imetolewa na:

SEDO Sekretariati
Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment