MBUNGE wa Kilwa Kaskazini Muktadha Mangungu, ameanza kuchimba visima 60 vitakavyogharimu zaidi ya Sh720 milioni, katika vijiji na shule za sekondari zenye tatizo la maji.Hatua hiyo inalenga katika kuwawezesha wapiga kura wake, kuondokana na kero ya muda mrefu ya kukosa huduma za maji. Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa uchimbaji wa visima hivyo, uliofanyika katika Shule ya Sekondari Ilulu, Mangungu alisema kwa muda mrefu, wananchi wa jimbo hilo wamekuwa wakikabiliwa na tatizo wa kukosa huduma za maji safi na salama. Alisema tatizo hilo limesababisha wananchi na hasa wanawake kutoshiriki vyema katika shughuli za maendeleo.Alisema mara baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge alipokea maombi mengi kuhusu mahitaji maji na Mangungu aliwaombwa wananchi katika jimbo hilo kumpa ushirikiano ili aweze kuwatumikia. Pia aliwataka kutumia vizuri visima hivyo ili viweze kudumu na kuwasaidia kwa kipindi kirefu.Kwa upande wake, mwalimu Sara Mlaponi wa Shule ya Sekondari Ilulu, alisema msaada huyo umekuja katika wakati mwafaka na kwamba utaweza kuondoa tatizo maji katika jumuiya ya shule hiyo. Alisema tatizo la maji, lilikuwa linawalazimisha wanafunzi kukatisha vipindi na kwenda kutafuta maji mtaani.
Chanzo - Mwananchi
No comments:
Post a Comment