Friday, September 16, 2011

Nahitaji Mawazo yenu kwa hili!

Kanali Joseph Simba Kalia  aliwahi kuwa  Mkurugenzi Mkuu wa National Development Corporation (NDC) yaani  Shirika la Maendeleo la Taifa ambalo lilisimamia mchakato mzima wa kuratibu na kusimamia  mradi wa Mtwara Development Corridor. Je ujio wake kwa mara nyingine kama Mkuu mpya wa Mkoa wa Mtwara unaleta sura gani kwa Wanakusini ukizingatia kuwa  Mtwara Corridor  imekuwa haieleweki na kuonekana kufa?

Kwa Maoni andika kusiniforum@gmail.com

1 comment:

  1. Kanali Simbakalia ni mfuatiliaji wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo. Kigoma alijitahidi ingawa atahitaji kuiendesha MT kisasa na si ki-Kigoma.

    Kuhusu Mtwara Dev Corridor, he has been very instrumental kwenye uanzishwaji wa mradi huu mkubwa. Akiwa Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa NDC, anaujua nje ndani na hata wanaouhujumu mradi huu yeye anawafahamu. Natumai wanakusini tutamwonyesha kuwa "Mtwara Dev Corridor ni mtoto wake" na hivyo sehemu ya Agenda zake kubwa iwe ufanikishaji wa utekelezaji wa mradi huu ambao unaonekana ndio ukombozi pekee wa kuamsha ari ya maendeleo kusini.
    Elimu na Mtwara Dev Corridor ndiyo ziwe agenda zake na sisi wanakusini tutampima mchango wake kwetu kutumia agenda hizi kuu mbili.

    ReplyDelete