Thursday, May 17, 2012

Umaskini wa Wananchi wa Kusini na Utajiri wa Gesi Asilia

Ni jambo lisilopingika kuwa hali ya kiuchumi na kimaisha ya wananchi wa kusini yaani mikoa ya Lindi na Mtwara ni duni mno ukilinganisha na baadhi ya maeneo nchini. Hali ya miundombinu ni ya kukatisha tamaa na ni ile ile miaka nenda rudi. Barabara nyingi za kutoka mikoani hadi wilayani ni za taabu na zinazounganisha wilaya na wilaya ndio usiseme. Huduma za jamii ni duni na mwanga wa maendeleo ya wanakusini bado haujaanza kuchomoza. Hali hii inaendelea kujikita hata wakati huu ambapo raslimali adimu na ya thamani kubwa ya gesi asilia iliyogunduliwa na kuanza kutumika zaidi ya miaka kumi sasa na matumaini ya kupatikana kwa mafuta yakiongezeka. Je, ilikuwa ni muda muafaka kwa Naibu Waziri mmoja katika ya wawili wa wizara ya Nishati na Madini ambaye anashughulikia raslimali ya gesi na mafuta atoke kusini ili kuhakikisha anapigania kuwekwa kwa utaratibu wa wazi ambapo wananchi wa kusini wananufaika na gesi na mafuta kama taratibu zilizowekwa kwenye maeneo mengine ambayo yana raslimali?

No comments:

Post a Comment