Friday, September 16, 2011

Mnaonaje kuhusu hili wadau?

Kwa nini Lindi mara nyingi huwepa Wakuu wa Mkoa ambao ni  Ma-DC wazamani na kuja kuanzia kazi za Ukuu wa Mikoa na kupatia uzoefu hapo? Je ni kwa nini wazoefu na wenye uzoefu hawapelekwi huko ukizingatia kuwa Lindi inahitaji mtu mwenye uwezo na uzoefu kutokana na maendeleo yake kuwa nyuma?

Kwa kuchangia mada hii andika kusiniforum@gmail.com

2 comments:

  1. Inauma kuona jambo hili hujitokeza mara kwa mara. Nakumbuka Mecky Sadiki alikuwa mkuu wa wilaya Mtwara wakati Lindi alikuwa Fatma Mikidadi (sasa mbunge viti maalum - CCM, Lindi). Baadae wakabadilishana baada ya ugomvi wa mpira kati ya Kariakoo )Lindi) na Bandari (Mtwara). Baadae Sadiki akapandishwa kutoka mkuu wa wilaya Lindi na kuwa mkuu wa mkoa Lindi.

    Ali Rufunga aliwahi kuwa mkuu wa wilaya Rufiji na Mafia au Kilwa. Na sasa anapelekwa Lindi kujifunzia kazi huko. Jamani mimi binafsi siridhiki kabisa na mwenendo huu. Lindi na Mtwara tunahitaji viongozi shupavu. La sivyo wakuu wa mikoa na wilaya tuwachague sisi wenyewe.

    ReplyDelete
  2. Its true 4 mr Rufunga he was the DC for masasi district,but he never delivered the expected goals.It our role to make them accountable

    ReplyDelete