Tuesday, September 27, 2011

Mjadala wa Leo 27.09.2011ndani ya SSQ huu hapa!

Nashukuru wadau kwa kuona kuna umuhimu kwa watu wa kusini kuwa na network yetu ya kubadilishana mawazo. Kwa upande wangu naungana na mdau mmoja ambaye aligusia suala la viongozi wetu kuwa wabovu. Lakini kitu ambacho mie nimekigundua ni taaluma ndogo ya hao viongozi wetu. Ebu tuangalie wabunge wetu wa kusini. Asilimia 90% ni form four failures au standard seven. Wakati Kilimanjaro mbunge mwenye elimu ndogo ni undergraduate (Degree). Sidharau elimu zao wabunge wa kusini ila tunafikiri upeo wao wa kuchambua mambo ukoje? - Jordan Nankoko

Noel Makwinya kaka Omar Makwinya, Sijagusia uwekezaji mkubwa ambao wengi wetu hatuuwezi. Shuka chini, nagusia mdogomdogo ambao utamtoa hata mtu wa kaskazini akaja kama ulivyomtua juma toka mtwara kumpeleka Mwanza. HIVI UMEWAHI KUFANYA UTAFITI KWA NINI WATU WA KASKAZINI HAWAJI KWETU WAKAKUAMBIA SABABU? THE OPPOSITE NDIZO ZINANOTUFANYA SISI TUENDE KWAO

Jennifer Livigha hayo ya usomi achana nayo, hapa tunajadili issue za maendeleo hatujauliza nani msomi au mjinga na hilo nalo ni tatizo shule zetu sio sababu ya kuona tofauti zetu , wewe unaweza kufaa kwa hili lakini pamoja na elimu yako ukashindwa kufaa kwa jambo lingine, ujinga wangu na werevu wako havitufanyi mimi na wewe kushiriki katika mjadalka wa kuleta maendeleo kusini hatuhitaji CV za watu hapa tunahitaji kuangalia nini tufanye kama wazawa katika kurekebisha wetu

Omar Makwinya Noel kujenga Tabata au kwingine kwangu its not a deal naamini hata kwa wengine wengi hapa issue ni kuwa wanfanya nini nyumbani kwani kwangu huku mjini ni kama ifetch out investiment from other place to our home place

Hassan Elias its too general kuanza kusema hapa nani kafanya nn au anatarajia kufanya nn kusini,hatushindani hapa tunazungumzia hali halisi ya maisha ya watu wa kusini,Noel unakumbuka wakati ule chuo watu wakusini tukiomba tukutane kuna watu walikuwa hawataki kujitambulisha wala kujulikana kuwa wanatoka mikoa ya kusini? nn sasa hata kuwaficha watu asili ya kwenu kama si ushamba hivi kuna ambaye hana kwao

Hassan Elias its too general kuanza kusema hapa nani kafanya nn au anatarajia kufanya nn kusini,hatushindani hapa tunazungumzia hali halisi ya maisha ya watu wa kusini,Noel unakumbuka wakati ule chuo watu wakusini tukiomba tukutane kuna watu walikuwa hawataki kujitambulisha wala kujulikana kuwa wanatoka mikoa ya kusini? nn sasa hata kuwaficha watu asili ya kwenu kama si ushamba hivi kuna ambaye hana kwao

Jennifer Livigha Hassan shaka ondoa mimi ni zaidi ya unavyofikiri ila ukifanya kipimo cha macho nafikiri utanipa maski ndogo ambazo binafsi sizimaind ahaaa

Noel Makwinya Dada Jennifer Livigha, sijagusia usomikumdharau mtu, soma vizuri mchango wangu. Nimesemaje juu ya hofu yako kuwa nina hasira na tofauti zetu, nimesema usomi wangu unanifanya nivumilie tofauti na niamini ndo chanzo cha jibu sahihi. Please, usije ukaniquote vibaya!

Noel Makwinya Kaka Omar Makwinya, ukisema hivyo utawaudhi watu! watu wanasisitiza TUKAJENGE KWETU NDO UZALENDO, we unasema SI TATIZO KUJENGA MBALI

Omar Makwinya Noel nyumbani kunajengwa kwa mambo mengi sana sio nyumba tu. Yawezekana ukaweza jenga Dar au kwingine lakini contribution yako kwa jinsi nyingine personally ikaweka gudumu highly speeded. Kwani wengine hujenga kwa kudeheni na kwa kimaghumashi na poia kuna vigezo

Omar Makwinya Bwa somo au wewe kujenga waelewa ni nyumba tu. Inakhava tulighanishia hibhanda jika kumbe kushipagwa yaigwinji

Jennifer Livigha issue ya kujenga Tabata au Mbagala na hata kenya sio tatizo tatizo wewe kama wakusini unaridhishwaje na mfumo mzima wa maisha wa ndugu zako wakliopo huko? kazi yetu kila siku kusifia oooh arusha kuzurii yaani kumejengeka sana ngoja nitafute hela na mimi nikakanunue kiwanja Njiro ahaaa shame on you kwa yoyote anayefanya hivyo na kukataa asili yake

Noel Makwinya Kaka Omar Makwinya, mi nimelipigia kelele sana hilo, soma old posts na contribution zake ndo utaona kama unachosema nimekisemea sana. Na hii ndo mada ninayoipigia kelele juu ya uwekezaji, nikiamini kuwekeza nyumbani ndo uzalendo na si kusimamisha vibanda halafu basi. Umenielewa?

Jennifer Livigha noel unataka wasio wasomi hawajui kudhibiti hasira zao? kuna degree ya kudhibiti hasira? jaribu kuwa na uchmbuzi wa maneno wakati unaongea na mtu zaidi ya mmoja coz kila mtu anaupeo wake wa kuelewa next time utajikuta unaeleweka vizbaya kama utashindwa kupanga maneno yako, sio watu wote tuna elimu na upeo kama wako Noel try to be naturaly maongezi mengine hayahitaji shule

Noel Makwinya ‎@ Dada Jennifer sijakuelewa, naona kama unajicontradict

Hassan Elias Noel si kweli kwamba watu wakaskazini hawaji kusini,mathalani ukiondoa wamakonde ndugu zetu,wafanyabiashara wote wakubwa Nachingwea na kwingineko ndani ya kusini ni wakuja tu,wachaga wamejaa kibao,wakinga nk na ndio wanatoa huduma kwa ndugu zetu,kama wao wanaweza kufanya hayo huku ss ni yepi yanayotusibu?

Noel Makwinya Kama maneneo yangu yamepokelewa kwa mtazamo wa kuwakera wasio wasomi, NAFUTA KAULI. Sina hasira na naamini tofauti za mawazo ndo huzaa jibu. USOMI HAUCHANGII KATIKA KUJUA HILI!

Noel Makwinya SAMAHANI SANA WANAKUSINI KWA KAULI YANGU KUWA MIMI NI MSOMI NINAYEAMINI KUBOREKA KTK TOFAUTI ZETU NA CONVISING

Jennifer Livigha huwezi kunielewa kwa sababu wewe unahisi tuna level tofauti

Omar Makwinya Mh, nyie watu kuweni makini na style yenu unajua unaweza sema Nakupenda kumbe pronouncing yako, au sentnsi yako ikimaanisha umekasirika na wamchuk

Jennifer Livigha usomi wako umeleta mabadiliko gani katika uchangiaji wa Elimu kusini ili uliowaacha kijijini nao waje kuelemika kama wewe?Noel

Noel Makwinya Dada Jenifer na wote mnaofuatilia majadiliano haya. Someni mchango wangu muone hilo neno analoshupalia dada Jenifer linatoka wapi. PENYE TATIZO NAOMBA RADHI, NA ISIENDELEE KUWA MADA. TURUDI KWENYE HOJA!

Jennifer Livigha sio kila asema bwana bwana ndio atayeuona ufalme wa mbingu , nimeamini kuwa ukubwa wa pua sio wingi wa kamasi ahaaaa

Hassan Elias kusoma ni pamoja na kujua wakati gani unazungumza na unazungumza na nani,uteuzi wa maneno na kauli ni viashiria vya mtu kuelimika

Omar Makwinya Hey Noel Idana tena J

Jennifer Livigha Noeli nikuulize swali?

Jennifer Livigha kwa Ulimwengu wetu huu wa KTZ utamjuaje kuwa huyu mtu ni Mhaya:

Noel Makwinya Jennifer Livigha, RUDI KWENYE HOJA YA MSINGI! UNATAKA NA HAPA PAWE NA MWONGOZO WA SPIKA? MBONA NIMESHAFUTA KAULI KWA MANUFAA YA SSQ?

Omar Makwinya Teh teh @Hassan

Jennifer Livigha nataka nikuambie kuwa kuna mtu utajua tabia na matendo yake kutokana na kauli zako kwani

Noel Makwinya Dalili ya kupevuka ni kuelewa mwenzio anachosema. Dalili ya busara ni kumwelewa anayekiri udhaifu pale inapolazimika. TURUDI KWENYE HOJA.

Hassan Elias turudi kwenye mjadala hayo ya usomi yameshaeleweka,au mmechoka mwamanganyanji?

Jennifer Livigha Binafsi nahisi ifike wakati watu wa kusini tujitambue na kujua thamani yetu mbele ya wengine na kuamini kuwa tunaweza kwani hata ROMA haikujengwa siku moja! Maendeleo ya kusini yataletwa na sisi wenyewe iwapo tutaona tunahitaji hayo maendeleo na sio lazima mimi au wewe kutoa hela ila kama utapaza sauti yako na wale wengine wakaisikia vizuri ujumbe utafika na watu watapata muamko na kuleta mabadiliko tutayotaka

Jennifer Livigha ahaaaaaaaa hassan unaniumiza tumbo naona umenirudisha matangazo Radio Tanzania Stesheni

Jennifer Livigha Noel una shida hata kama hutaki kuliona binafsi sina nia mbaya na wewe ila kama vile unavyojua watu wengi wa kusini hatuna shule so nilikuwa nakupa angalizo na hizo sentenzi zako za usomi, mimi sina shida coz huwa simpi nafasi mtu yoyote kunidharau mara zote hujipa nafasi ya kwanza na wengine hufuata hata kama ukina nani na unatoka wapi na unafanya nini kwangu you are second choice and i can remain the first ahaaaaa na kiingerreza changu cha kimwera msinicheke

Jennifer Livigha haasan lete mada au tuendeleze hii

Hassan Elias Noel uwa unanionea sana na umemkimbiza Hamisi mikate sasa je umeona eeh kwa dada jeny ? mpaka na kauli umefuta safi sana kwi kwi kwi kwi kwi!

Omar Makwinya Mikate hajakimbia ila hapendi mabishano na by the way mwepesi kugive up. Ila kama tukiwa wise tutajenga kwa pamoja na tunaweza

Jennifer Livigha ‎' TOGETHER WE CAN' ahaaaa

Noel Makwinya Dada Jennifer Livigha, tofauti yangu na yako katika hili nimeielewa, na nimeshalisemea. WEWE DADA UKOJE MBONA UNASHUPALIA TRIVIAL ISSUES? Mimi nina shida nakiri, wewe mkamillifu tena saaaana, yaishe basi TURUDI KWENYE HOJA! ee, dada, huko mtaani si wanakukoma!

Jennifer Livigha hayo umesema wewe kam wananikoma au hawanikomi ni wao na wewe kwangu si issue try to be naturaly bwana Noel hayo mambo yako ya you know or ahaaa its old fashion big brother

Jennifer Livigha Binafsi nipo tofauti na unavyofikiri namshukuru Mungu na laiti kama ungenijua ingekusaidia kunielewa sijawahi kubadilika na huwa naomba maisha au hali ya hewa isibadili mwendo mzima wa tabia yangu ahaaa

Hassan Elias uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii mbavu zangu,dada jeny na noel inatosha .im out love u all c u jioni for another issue

Jennifer Livigha Lete Mada Nyingine Neol Thanks kwa Jordan Nankoko kwa kuanzisha mada hii leo , My self, Hassan Elias, OmaryOmar Makwinya na very special kwa wewe Noel at last tumejuana kwa kiasi fulani a big interview with each other aahaaaaa

Was so emmotional uwwwww - Jennifer
Jennifer Livigha Jamani naweza kupost hizi issue kusini forum zilete changamoto

No comments:

Post a Comment