HALMASHAURI ya Manispaa ya Wilaya ya Ilala imeanza kuvunja makufuli katika vizimba vya Soko la Machinga Complex, ambavyo wamiliki wake hawajaanza kufanyia biashara. Kuvunjwa kwa vizimba hivyo, kumekuja baada ya wafanyabiashara hao kukaidi amri ya manispaa hiyo, inayowataka waanze kuvitumia ili kuondoa malalamiko kutoka kwa wafanyabishara wengine waliovikosa. Agizo hilo la kuvunja makufuli, lilitolewa wiki iliyopita na Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko hilo, Abubakar Rakesh, baada ya vizimba hivyo kukaa wa muda mrefu bila vikiwa havina bidhaa, jambo ambalo limeibua malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara waliokosa maeneo. Kazi ya kuvunja makufuli hayo iliyoanza mwishoni mwa wiki iliyopita na kusimamiwa na Meneja wa soko hilo, Teddy Kundi, chini ya ulinzi wa polisi. Teddy alisema vizimba ammbavyo makufuli yake yamevunjwa ni vya wamiliki ambao hawapo. Hata hivyo aliwataka wamiliki wa vizimba hivyo ,kufuata bidhaa zao katika ofisi za Manispaa ya Ilala na kulipia gharama za uvunjaji , kodi ya miezi ambayo vizimba havikufunguliwa na gharama za kuhifadhi bidhaa. “Mizigo yao ipo , ndani ya siku thelathini wawe wamekuja kuchukua na kulipia gharama za uvunjaji, kodi wanazodaiwa na gharama ya kuhifadhi mizigo yao,”alisema Teddy.
Chanzo - Mwananchi
Ni kweli maana Machinga Complex haikuwa ya wamachinga tunaowajua ila vigogo na ndugu zao. Tuwape nafasi vijana na tuwaboreshee mazingira yao ya biashara kama tunavyoboresha ya wawekezaji kutoka nje ya nchi
ReplyDelete