Thursday, September 15, 2011

Happy Birthday Humphrey Paya!

Jana tarehe 14, septemba ilikuwa kumbukumbu yangu ya siku ya kuzaliwa (birthday)  na kwamba nimefikisha umri wa miaka 40.Ujumbe wangu kwa watu wa Kusini ni kuwaomba kuendeleza Moyo wa Uzalendo wa kupenda nyumbani,Aidha nimekutana na uzoefu kwamba Halmashauri za wilaya ambazo zinapaswa kusaidia maendeleo ya wananchi wetu hasa kwa masuala ya Elimu hazitekelezi wajibu wao ipasavyo, wanafunzi ambao wanasomeshwa na halmashauri hizo wanaachwa bila ya kusaidiwa au kuendelezwa wanapohitimu masomo yao hata kama wamefaulu masomo yao vizuri,iwe masomo ya sayansi ambayo yantuwezesha kupata wataalam wa afya ambao ni Aadimu sana hasa maeneo ya vijijini.Wanafunzi wengine wamefikia hatua ya kuwa waadhiri wasaidizi katika vyuo vikuu lakini hawakupata msaada stahiki na halmashauri zao.Hoja yangu kwenu ni kupata maoni yenu juu ya namna ya kufikisha hoja hii kwa wahusika ili ifanyiwe kazi.Namna nyingine ni kuanzisha Fund kupitia Sedo ili itumike kusaidia vijana genious ambao wazazi wao hawana uwezo.

1 comment:

  1. Kaka Happy birthday na Mungu akuzidishie umri, akili, busara, hekima na karama nyingi.Wazo lako ni excellent. Tuanzishe kampeni ya "Rudisha Elimu Kusini" ambapo tutachnagia na kuanzaa matamasha kusini kutoa elimu na shinikizo ili watendaji wasimamie maendeleo ya Elimu na huduma zingine ipasavyo. wadau mwasemaje? leteni mawazo

    ReplyDelete