Friday, August 19, 2011

Karibuni wotee www.kusiniforum.blogspot.com

Kwa kipindi kirefu tumekuwa tukitamani kuwa na sehemu au kitu kitachotufanya kituunganishe na kuona kuwa chetu au ni sawa na kuwa nyumbani,  nafikiri sasa wakati umefika kwa jamii yetu ya watu wa kusini (LINDI na MTWARA) kuungana na kujumuika pamoja kwa nia na madhumini ya kuleta maendeleo ya kwetu kwani " THAMANI YA MTU NI KUJENGA NA KUENDELEZA KWAO" kwa  heshima na taadhima napenda kuwakaribishwa watu wote wa kusini kwenye ukurasa huu ambao utakuwa kama sehemu ya makutano na jumuiko la kufanya ndoto zetu zitimie , ni imani yetu kuwa "KIDOLE KIMOJA HAKIVUNJI CHAWA na 
"PAMOJA TUNAWEZA"

Geoffrey Mwambe 
Chairman - SEDO Kusini

2 comments:

  1. Wadau wa kusini napenda kuwaarifu kuwa taasisi yetu ya kusini SEDO jana tar 23 Aug 2011 ilitimiza miaka minane (8) tangu ilipoanzishwa pale kwenye ukumbi wa Viwanja vya Saba saba kwa Mwl Nyerere Trade Fair. Taarifa hii haikuweza kuletwa kwenu jana kutokana na sababu za kiufundi. Tuwe pamoja ili tuijenge Lindi na Mtwara

    ReplyDelete
  2. Wadau wa kusini, naomba mtu atakayejitolea kuwa mratibu wa vikao vya kuwakutanisha wanakusini kama ifuatavyo:
    1. Mratibu - DSM
    2. Mratibu - Mtwara
    3. Mratibu - Lindi
    4. Mratibu - Mikoani
    5. Mratibu - Diaspora (Nje ya nchi)

    Naomba watakaojitolea watume e-mail kwa: mwambe.geoffrey@yahoo.com au kusiniforum@gmail.com.

    Majukumu ni:
    1. Kuwaunganisha wanakusini kwa kuwatafuta na kukusanya maoni yao
    2. Kuandaa vikao vya wanakusini km forum ya kujadili kero, fursa na mikakati ya maendeleo nyumbani
    3. Kuandaa program, kuhamasisha na kukusanya michango ya maendeleo
    4. Kujiweka pamoja na kusaidiana kwa hali na mali kwenye shughuli za msingi za maendeleo yetu

    Geoffrey Mwambe
    Chairman - SEDO Kusini

    ReplyDelete