
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye utiaji saini mkataba wa miradi ya Makaa ya Mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga, baina ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya nchini China, uliofanyika kwenye ukumbu wa Mlimani City Dar es Salaam, leo Septemba 21.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika Bendera maalum ya kumbukumbu ya watu wa China, wakati Mwenyekiti wa Bodi ya NDC, Christant Mzindakaya (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya China, Liu Canglong, (kushoto) wakisainiana mkataba

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akishuhudia zoezi la utiaji saini na kubadilishana mkataba

Zoezi la Kusaini Mkataba likiendelea

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya Sichuan Hngda Corporation Ltd, Liu Canglong, baada ya kuhudhulia zoezi la utiaji saini mkataba

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) Christant Mzindakaya, nje ya ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam leo Septemba 21, baada ya kumalizika kwa zoezi la kutiliana saini mkataba
No comments:
Post a Comment