Taasisi ya maendeleo ya mikoa ya Lindi na Mtwara (SEDO) inaandaa zoezi la kutambua mahitaji halisi ya idadi ya waalimu, masomo yenye uhitaji mkubwa wa waalimu na kiwango cha uandaaji wa kupokea waalimu kwenye shule za sekondari (hasa za Kata) katika mikoa hii. Waalimu hawa watapelekwa kama sehemu ya mpango wake wa kuinua kiwango cha elimu kusini ambacho kwa miaka kadhaa SEDO imekuwa ikiufanya kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa maendeleo ya mikoa yetu.
Wadau wote wa kusini mnaombwa kutoa ushirikiano wa hali ya juu ili kufanikisha lengo lililokusudiwa la kuokoa vipaji na kusaidia kupatikana na unafuu wa maisha kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Kila mmoja atimize wajibu wake na maendeleo kusini yatapatikana.
Mwenye mawazo, taarifa na mkakati wa kuboresha zoezi hili na la ufundishaji anaombwa asisite kulijadili kwenye KF, maana ndicho chombo chetu wanakusini.
Imetolewa na SEDO Sekretariati, DSM
Tarehe: 25 Jan 2012
No comments:
Post a Comment