Hali ya barabara za kuifikia mikoa ya Lindi na Mtwara imeendelea kuwa kitendawili na kuwa ndio chanzo kikuu (ukiachia vyanzo vingine) vya kuletezea uduni wa maisha ya wananchi wengi wa mikoa hii.
Kipande cha Ndundu-Somanga, ambayo ni kilomita 60 tu, kuelekea Lindi kutoka Dar es Salaam si tu ni kero lakini pia ni chanzo cha umaskini kwa wanakusini. Kama tujuavyo uhusiano wa DSM na mikoa ya kusini si tu kwa bidhaa za matumizi ya kila siku ila kwa masoko ya korosho, ufuta na karanga toka kusini.Ubovu wa barabara hii husababisha bei ya bidhaa madukani kuwa za juu kuliko maeneo mengi nchini ingawa kipato chetu ni kidogo kutokana na hali barabara kuongeza gharama za usafirishaji wa mazao yetu. Wanachi wa kusini wataweza kweli kusomesha watoto wao, kula na kupata huduma duni za matibabu?
Barabara ya Mangaka-Namtumbo Songea nayo ni tatizo kwani mahindi na maharage hutufikia kusini vikiwa bei juu.
Swali: Je, mikakati ikoje na sisi wanakusini tunawezaje kusaidia hali hii isizidi kutupelekea kwenye umaskini uliotopea maana hata waganga wa kienyeji sasa wanaonekana wana umuhimu kila tukiugua? Tuuze ardhi?
No comments:
Post a Comment