Saturday, October 15, 2011

Watakiwa kukopa mamilioni kwa kasi

WAJASIRIAMALI mkoani Lindi wameshauriwa kutumia fursa zinazopatika kwenye  Shirika la Viwanda Vidogo la Maendeleo (Sido) kama vile kukopa ili kuleta maendeleo yao na taifa kwa ujumla. Wajasiriamali 24 kutoka Wilaya ya Ruangwa  walitakiwa kufanya hivyo wakati wakikabidhiwa hundi ya thamani ya Sh11.5  milioni. Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, Hawa Mchopa aliwataka  wajasiliamali kujenga utamaduni wa kurejesha mikopo kwa wakati na kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa. Mchopa alisema tatizo kubwa la wajasiriamali wengi ni woga wa kuthubutu na  dhana potofu za kuogopa kukopa na kusababisha  washindwe kuchangamkia fursa zilizopo Sido. “Kwa sasa wananchi  wengi wana woga wa  kukopa kwa kuwa hawana utamaduni wa kulipa mikopo kwa wakati, nikosa kutorejesha,” alisema. 
Naye Meneja wa sido Mkoa wa Lindi,  Kasisi Mwita alisema shirika limetoa mikopo 1,301 yenye thamani  ya Sh550 milioni kwa kipindi cha miaka saba tangu 1994 mpaka Oktoba 2011 kupitia mifuko ya wafanyabiashara, wakulima na viwanda. Mwita alisema mikopo iliyotolewa kwa upande wa kilimo ni 341 viwanda 128, biashara 1,012, ufugaji 62, uvuvi 24, madini 14 na huduma nyingine walipewa mikopo 31. Wakizungumza kwa niaba ya  wajasiriamali wenzao, Abdalah garasi kutoka wilayani Ruangwa,  Moza Adinan na Ruakia Manzi walisema mikpo hiyo itawasaidia kuendeleza biashara zao  na kuinua hali yao ya maisha. Abdala garasi alisema wamepewa mikopo wakati  wa msimu wa zao la korosho na kwamba watazitumia kuzalisha na kuzaa faida, ambayo itasaidia  kurejesha mkopo kwa wakati.

Chanzo - Mwananchi

No comments:

Post a Comment