Friday, December 02, 2011

SEDO yajidhatiti kuinua kiwango cha Elimu Mikoa ya Lindi na Mtwara

Wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara kupitia taasisi yao ya maendeleo ya South Eastern Development Organization (SEDO) wamedhamiria kujikita kwenye kuinua hali ya maendeleo ya mikoa hiyo katika mppango wake wa maendeleo ya muda mfupi, kati na mrefu.
Hayo yalielezwa na uongozi wa SEDO katika maandalizi ya hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili hiyo hivi karibuni. Katika hafla hiyo, SEDO ilialika wadau mbali mbali wa maendeleo wakiongozwa na mawaziri na wabunge wanaotoka katika mikoa hiyo. Hafla hiyo ambayo ilifanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam ilihudhuriwa na mgeni rasmi Mh. Mustafa Haidi Mkullo, Waziri wa Fedha wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Uongozi wa SEDO ulibainisha wazi kuwa lengo lilikuwa kukusanya jumla ya Shilingi za kitanzania 150 milioni kwa ajili ya kugharamia waalim wanafunzi watakaopata nafasi ya kwenda kufundisha shule za sekondari (zikiwemo za kata) katika mikoa yetu.
Taarifa na picha za matukio zitafuata punde.

Chanzo: SEDO, Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment