Tuesday, July 31, 2012

Serikali Yalifungia Gazeti la Mwanahalisi

SERIKALI ya Jamhuri ya Tanzania, imelifungia gazeti la Mwanahalisi kwa muda usiojulikana kwakile kilichoelezwa kuwa na mwenendo wa kuandika habari na makala za uchozezi.

Sababu nyingine ya kufungiwa kwa gazeti hilo ni pamoja na kujenga uhasama na uzushi likiwa na nia ya kusababisha wananchi kukosa imani na vyombo vya dola hali inayoweza kuhatarisha amani na mshikamano wa nchi.

Akisoma tamko la Serikali leo jijini Dar es salaam, Kaimu Mkurugenzi Wizara ya Habari (MAELEZO), Phabian Lugaikamu, alisema kuwa katika toleo la gazeti hilo namba 302, 303 na 304 ya mwaka 2012 na mengine yaliyotangulia yalichapisha habari na makala zenye kueneza na kujenga hofu kwa jamii.

“Mhariri wa gazeti la Mwanahalisi ameitwa na kuonywa mara nyingi lakini hataki kukiri kuwa maudhui ya makala zake hazina tija kwa jamii,pia hazifuati weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari”alisema Aidha alisema kuwa mhariri huyo mara zote katika utetezi wake amekuwa akinukuu kifungu cha 18 cha katiba ya nchi kinachotoa uhuru wa kutoa maoni na kwa makusudi kutokunukuu kifungu ca 30 cha katiba hiyo kinachoweka ukomo wa uhuru.

“Serikali imeamua kulifungia gazeti hilo kutochapishwa kwa muda usiojulika kwa mujibu wa sheria ya magazeti ya mwaka 1976, kifungu namba 25(i),adhabu hiyo itaanza tarehe 30 julai,2012 kwa mujibu wa tangazo la serikali namba 258 lililochapishwa katika gazeti la Serikali na kutolewa jijini Dra es salaam julai 27,2012”alisema.

Wapendekeza Katiba Mpya Ifute Muungano

MUUNDO wa sasa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,unapaswa kufanyiwa marekebisho kupitia Katiba Mpya, ili kupunguza manung’uniko na hatimaye mwafaka kuhusu Muungano.
Hayo yalisemwa juzi na wananchi wa Jiji la Tanga, walipokuwa wakitoa maoni yao kwa Tume ya Kukusanya Maoni ya Wananchi kuhusu Mabadiliko ya Katiba Mpya.

Wananchi hao, wamedai kuwa muundo wa sasa wa Muungano hauna tofauti na kuwaunganisha tembo na sungura, jambo ambalo haliletin usawa.


Akitoa mapendekezo yake, Jonathan Bahweje alisema kimsingi muundo wa sasa wa chombo hichon haufai kwa sababu hakuna fursa sawa kati ya Zanzibar na Tanzania bara.

“Muungano wa sasa ni kama tembo na sungura, unawaweka pamoja halafu unasema umewaunganisha na wako sawa, wakati kwa uhalisia, haiwezekani,” alisema Bahweja.

Mwananchi huyo alipendekeza Katiba Mpya, ivunje muungano ili usiwepo
hatimaye Tanzania bara na Zanzibar, kila moja ijitegemee na kwamba hakuna sababu ya kuogopa kuuvunja chombo hicho.

“Mimi napendekeza Muungano uvunjwe ili kila nchi iwe na Serikali yake, kwa sababu manung’uniko ni mengi na yanayotokana na jinsi muundo wa sasa usivyokubalika,”alisema Bahweja.

Alisema kama kuna ugumu wa kuvunja Muungano, basi ni vema kukawa na Serikali tatu, ili kila nchi iweze kuwa na uhuru wa kuendesha mambo yake wakati kuna Serikali ya Muungano itakayosimamiwa masuala yanayohusu Muungano tu.

Kwa upande wake, Rashid Juma, ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Kivumbitifu, katika Kata ya Pongwe, alitaka Muungano uvunjwe kwa madai kuwa wananchi wa Tanzania bara wanapokwenda Zanzibar na kurejea na bidhaa, wanatozwa ushuru wakati wakiwa ndani ya nchi moja.

“Huu Muungano hauna faida kwetu wananchi wa Tanzania bara, unasemaje wamba tumeungana lakini sisi tukienda Zanzibar tukija na bidhaa tunatozwa ushuru lakini ukipeleka kutoka bara hakuna ushuru,”alihoji Jumaa.

Source: Gazeti la Mwananchi

Thursday, June 28, 2012

TPDC NA BOMBA LA KUSAMBAZA GESI VIWANDANI, MAJUMBANI




Baadhi ya mabomba yatakayotumika kusambaza gesi viwandani na majumbani likiwa limetandazwa chini ya ardhi na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC). Picha na Joseph Zablon.

PEMBEZONI mwa barabara ya Mandela, jirani na eneo la biashara la Mlimani City, mafundi wanatandaza mabomba katika mrefeji uliochimbwa kutoka Ubungo mpaka katika eneo hilo.
Mabomba hayo inaelezwa kuwa ni ya kusambaza umeme wa gesi viwandani na majumbani na mpango huo unaratibiwa na kusimamiwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC). Mpango huo wa awamu ya kwanza unatarajiwa kukamilika Juni mwaka huu.

Kukamilika kwa utandazaji wa mabomba hayo kutatoa fursa kwa Mlimani City, nyumba 57 na viwanda sita vilivyopo eneo la Mikocheni, kuanza kutumia umeme wa gesi. Mabomba hayo yatatadazwa kwenye maeneo mengine, jijini Dar es Salaam.

Gesi kusambazwa majumbani
Kulingana na ripoti ya utendaji ya TPDC ya mwaka 2011, Kampuni ya Ushauri Welekezi ya Ms. Ultimate Petroleum Technology mwaka 2007 ilikamilisha upembuzi yakinifu wa mpango wa kusambaza gesi majumbani, mahotelini na kwenye magari katika Jiji la Dar es Salaam.

Upembuzi huo umekusudia kujenga mtandao wa mabomba makubwa kando ya barabara zote za Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kusafirisha gesi. Pia ujenzi wa vituo 12 vya kujaza nishati hiyo katika magari.
Pia mpango huo umelenga magari 8,000 na nyumba 30,000 na gharama za mradi zinatajwa kufikia dola 55 milioni za kimarekani mpaka kumalizika kwa mpango huo. Awali walitenga dola 30 milioni kwa ajili kukamilisha mtadi huo.

Kuanzia mwaka jana mpaka sasa viwanda 35 zikiwamo nyumba 17 ambazo zipo kwenye mradi wa majaribio vinatumia nishati hiyo.

Kutokana na kampuni hizo zimeokoa dola 187 milioni za kimarekani baada ya mwaka jana kuanza kutumia gesi.

"Fedha hizo zingetumika iwapo wangetumia mafuta ya petroli na dizeli" inasema sehemu ya taarifa ya TPDC ya utekelezaji wa mradi huo.
Tangu mwaka 2004 mpaka mwaka jana Serikali imepata Sh114 milioni kutokana na mauzo ya gesi.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa kusudio la matumizi ya umeme wa gesi ni kupunguza matumizi ya nishati asili kwa mfano, mkaa, kuni na mafuta mengine yanayoagizwa kutoka nje ya nchi kwa ajili ya nishati. Umeme unaozalishwa na gesi asilia ni megawati 341.

Pia ripoti hiyo inabainisha kwamba hivi sasa mabomba yanatandazwa kwa ajili ya kusambaza gesi katika eneo la biashara la Mlimani City na maeneo ya jirani.

Baada ya mpango huo kukamilika kutakuwapo na ongezeko la watumiaji wa umeme utokanao na gesi.
"Hivi sasa Serikali inaweka mkazo katika uzalishaji wa umeme wa gesi kuliko ule wa maji (hydropower)" inasema taarifa hiyo.

Mahotelini ni kati ya maeneo ambako umeme wa nishati ya gesi asili, utasambazwa.
Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, John Ngeleja anasema mpango huo ulianza kutekelezwa jijini Dar es Salaam kutokana na jiji hilo kuwa na mahitaji makubwa ya umeme kuliko miji mingine Tanzania.
Pia mpango umetekelezwa Dar es Salaam kwa sababu maeneo yake, yamepimwa na kuacha nafasi ya kupitisha mabomba hayo kwa ajili ya mradi huo.
Mpango huo utasambazwa Mkoa ya Lindi ambako gesi hiyo inazalishwa kadiri mradi utakavyozidi kupanuka.

Ofisa Mtafiti katika Kurugenzi ya Masoko na Uwekezaji, Emmanuel Gilbert anasema mradi wa kutandaza mabomba ni tofauti na ule wa majaribio ambao unatekelezwa hivi sasa katika nyumba 17 za wafanyakazi wa TPDC Mikocheni na katika viwanda 35 kikiwamo cha Saruji cha Twiga, kilichopo eneo la Wazo.

Anayataja maeneo ambayo yapo katika awamu ya pili ya mradi huo ni Chuo cha Maji Rwegarulila hadi Chuo Kikuu Dar es Salaam.
Mabomba mengine anasema yatafungwa katika matoleo yaliyopo kona ya kuelekea eneo la Sinza kutoka barabara ya Sam Nojuma na katika makutano ya Ali Hassan Mwinyi na Sam Nujoma kwa ajili ya Kambi ya Jeshi Wananchi Lugalo na watu wanaoishi kambini humo.

Umeme wa uhakika kupatikana
Gesi ya asili ilianza kuzalisha umeme Julai 2004, katika mitambo ya Shirika la Ugavi Nchini (Tanesco) Ubungo. Katika mpango huo walianza kuzalisha megawati 151 na mpaka sasa nyumba 17 pekee zinatumia nishati hiyo kwa majaribio katika eneo la Mikocheni.
Gilbert anasema lengo la mradi ni kupunguza umeme wa maji ambao siyo wa uhakika kutokana na uhaba wa mvua na kwamba mpango huo utawawezesha kupata umeme kwa bei ya chini tofauti na sasa.
Pia mradi umelenga kupunguza matumizi ya nishati ya kuni na mkaa. Takwimu za Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), zinabainisha kwamba zaidi ya magunia 40,000 ya mkaa yanatumika kila siku katika Jiji la Dar es Saalam.
Kiwango hicho ni tofauti na kile ambacho kinatumika mikoa mingine nchini na kiasi cha mkaa ni tofauti na nishati ya umeme na nchini kwani kwa siku megawati 850 zinahitajika kuzalisha umeme.
Wakati mwingine megawati hizo zinashuka na kufikia megawati 600 na kusababisha mgawo wa umeme nchini kutokana upungufu wa maji katika mitambo ya kuzalishia umeme inayotumia mvua.
Pia mradi huo unatarajiwa kupunguza matumizi ya fedha za kigeni kwa ajili ya kununua aina nyingine za gesi na mafuta kutoka nje ya nchi.
Umeme wa gesi asili unatarajiwa kupunguza uharibifu wa misitu na uchafuzi wa mazingira.

Ofisa huyo anasema mpango huo umelenga kujenga mtandao wa mabomba makubwa kando ya barabara zote za Jiji la Dar es Salaam na ujenzi wa vituo vitatu vya kushindilia gesi katika mitungi, vituo 12 vya kujaza gesi kwenye magari.

Anasema mradi huo utagharimu dola 55 milioni za Marekani mpaka utakapokamilika. Fedha hizo ni pamoja na vyanzo vingine pia zinatokana na gawio la asilimia 50 ya mauzo ya gesi nchini kutoka serikalini.

Gilbert anasema ujenzi wa bomba la kilometa saba kutoka Ubungo hadi Mikocheni upo katika hatua nzuri na kituo cha gesi kilichopo katika hoteli ya Serena ambacho kinasambaza katika hoteli zingine pia na cha Ubungo vinatoa tija. Anasema bomba la Ubungo lina ukubwa kutosha kulingana na mahitaji ya baadae ya nishati hiyo kwa wateja. Anasema baada ya bomba lingine la Mtwara mpaka Dar es Salaam kukamilika litaongeza usambazaji wa nishati hiyo kwa watumiaji.

Vituo vya kuuzia gesi
Gilbert anasema watumiaji wa gesi watakuwa wakilipia huduma hiyo kwa Luku. Wakazi watafungiwa mashine na kununua uniti katika vituo vilivyokusudiwa.

Bei ya kuuzia gesi ipangwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mafuta na Gesi (Ewura) na kwamba nishati hiyo ya umeme inauzwa kwa bei ya chini kuliko nyingine nchini.

Pia umeme huo ni rahisi kuliko mwingine na kwamba bei ya kuuza umeme huo umepangwa sawa na bei ya kipimo cha kopo la mkaa na kutoa punguzo la asilimia 20 kwa bei iliyopo sokoni.
"TPDC ni chombo cha Serikali hivyo bei zake tumekokotoa kwa kuwianisha na bei za nishati zingine ambazo zinatumiwa na wananchi wengi ambazo ni kuni na mkaa," anasema.

Habari na Joseph Zablon
Chanzo - http://www.mwananchi.co.tz

Sunday, June 17, 2012

Labda wakati huu Wanakusini tuaminishwe ... na hili kuhusu barabara ya Ndundu - Somanga (Govt: Ndundu-Somanga road to be completed next fiscal year)

14th June 2012 Construction of the 60-kilometre road from Ndundu in Coast region to Somanga in Lindi region at tarmac level will be completed next financial year (2012/13), the National Assembly was told here yesterday. Works deputy Minister Gerson Lwenge assured the House when responding to question by Fatuma Abdallah Mikidadi (Special Seats), who wanted to know when construction of the Kibiti-Lindi–Mingoyo road, which she described as long overdue, would be accomplished. The lawmaker also wanted the government to explain the reasons for the overdue delays in the completion of the road, which is the main link of the Southern Corridor. Lwenge told the House that currently 284 kilometers of 344 kilometers have been accomplished and the remained 60 kilometers will do in the next financial year. The deputy minister noted that so far the government had paid the contractor undertaking the construction, M/S Kharafi, a total of 45bn/- and the total cost of the road’s construction was projected at 59bn/-. Lwenge added that it was the sole responsibility of the contractor to make regular repair of the road as well as ensuring that it was passable all the time. Construction of the Kibiti-Lindi highway started in 1974 during Mwalimu Nyerere’s reign. Despite its pivotal role of linking Tanzania and southern African countries, particularly Mozambique and Malawi, the building works had taken almost forty years.. He said it was true that the 60-kilometre-long road had taken a number of years to be completed and inconvenienced the people living and going to southern regions. According to him, already 20 kilometres of tarmac road had been completed. “The government is aware of the problems which people in the southern regions are facing. We are taking measures to make sure that the contractor completes his assignment during the 2012/2013 financial year,” he affirmed. In her basic question, the MP had said that the Kibiti-Lindi road played a crucial role in the development of the Southern Corridor and linked Tanzania with the countries of Malawi, Mozambique and South Africa. She therefore wanted the government to explain when the road’s construction would completed. SOURCE: THE GUARDIAN

Friday, May 18, 2012

Kila la Kheri Wadau wa SEDO kwenye Majukumu Mapya

Uongozi wa SEDO unachukua nafasi hii kuwapongeza wadau wake walioteuliwa hivi karibuni kubeba dhamana za kuongoza wilaya mbali mbali nchini ambao ni: 1. Dr. Nassor Hamid (Lindi) 2. Yahya Nawanda (Iramba) 3. Elias Hassan Masala (Kilombero) 4. Mh. Agnes Hokororo (Ruangwa) 5. Shaibu Ndemanga (Mwanga) 6. Suleimani Kumchaya (Tabora) 7. Abdula Lutavi (Namtumbo) 8. Said Amanzi (Morogoro) Tunawatakia kila la kheri na waoneshe uwezo uliotukuka katika kuwaletea maendeleo wanaowaongoza. SEDO Sekretariati Dar es Salaam

Thursday, May 17, 2012

Umaskini wa Wananchi wa Kusini na Utajiri wa Gesi Asilia

Ni jambo lisilopingika kuwa hali ya kiuchumi na kimaisha ya wananchi wa kusini yaani mikoa ya Lindi na Mtwara ni duni mno ukilinganisha na baadhi ya maeneo nchini. Hali ya miundombinu ni ya kukatisha tamaa na ni ile ile miaka nenda rudi. Barabara nyingi za kutoka mikoani hadi wilayani ni za taabu na zinazounganisha wilaya na wilaya ndio usiseme. Huduma za jamii ni duni na mwanga wa maendeleo ya wanakusini bado haujaanza kuchomoza. Hali hii inaendelea kujikita hata wakati huu ambapo raslimali adimu na ya thamani kubwa ya gesi asilia iliyogunduliwa na kuanza kutumika zaidi ya miaka kumi sasa na matumaini ya kupatikana kwa mafuta yakiongezeka. Je, ilikuwa ni muda muafaka kwa Naibu Waziri mmoja katika ya wawili wa wizara ya Nishati na Madini ambaye anashughulikia raslimali ya gesi na mafuta atoke kusini ili kuhakikisha anapigania kuwekwa kwa utaratibu wa wazi ambapo wananchi wa kusini wananufaika na gesi na mafuta kama taratibu zilizowekwa kwenye maeneo mengine ambayo yana raslimali?

Tuesday, May 15, 2012

Wajue Wakuu Wapya wa Wilaya za Kusini

Wakuu wetu wapya wa wilaya ni hawa wafuatao wakiwemo wanachama wa SEDO: A: Mkoa wa Lindi: 1. Dr. Nasoro Ali Hamidi (Lindi) 2. Ephraem Mfingi Mmbaga (Liwale) 3. Mh. Agness Hokororo, Mbunge Viti Maalum - Mtwara (Ruangwa) 4. Ulega H. Abadallah (Kilwa) 5. Regina Chonjo (Nachingwea) A: Mkoa wa Mtwara: 1. Farida S. Mgomi (Masasi) 2. Christopher Magala (Newala) 3. Festo Kiswaga (Nanyumbu) 4. Wilman Kapenjama Ndile (Mtwara) 5. Ponsiano Nyami (Tandahimba) Una lipi la kumwambia mkuu wako wa wilaya ambayo ungependa ayashughulikie kwa ustawi wa watu wetu? SEDO inafanya mpango wa kuwa na mawasiliano nao ya mara kwa mara ili kujuza kero za wanakusini kwenye maeneo yao ya kazi. Tafadhali "tufunguke" ili wajue kusini ina wenyewe.

Friday, May 11, 2012

Baada ya Kimya Kirefu hatimaye JK Ateua Wakuu Wapya wa Wilaya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete amewateua wakuu wapya 70 na kuwabakiza wa zamani 63 kuongoza wilaya 133 nchini ikiwa ni mwaka mmoja na miezi sita baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa 2010. Katika uteuzi huo ambao majina ya wateuliwa yalitangazwa na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiambatana na Waziri wa TAMISEMI Mh. Hawa Ghasia na Naibu wake Mh. Aggrey Mwanri, Rais ameteua vijana wa kike na wa kiume kadhaa wenye umri chini ya miaka 35 ikiwa ni moja ya mkakati wa CCM na Serikali kurithisha vizazi uongozi wa nchi. Katika uteuzi huo, majina kadhaa ya walioanguka kwenye uchaguzi uliopita katika ngazi ya ubunge na wataalamu mbali mbali wakiwemo madaktari wa binadamu. Katika uteuzi huo ambao umewaacha nje wakuu wa wilaya wa zamani 51, umeshuhudia karibu wilaya mpya 19 zikiundwa. Orodha kamiliya walioteuliwa ni kama ifuatavyo: 1. Novatus Makunga Hai 2. Mboni M. Mgaza Mkinga 3. Hanifa M. Selungu Sikonge 4. Christine S. Mndeme Hanang 5. Shaibu I. Ndemanga Mwanga 6. Chrispin T. Meela Rungwe 7. Dr. Nasoro Ali Hamidi Lindi 8. Farida S. Mgomi Masasi 9. Jeremba D. Munasa Arumeru 10. Majid Hemed Mwanga Lushoto 11 Mrisho Gambo Korogwe 12. Elias C. J. Tarimo Kilosa 13. Alfred E. Msovella Kiteto 14. Dkt. Leticia M. Warioba Iringa 15. Dkt. Michael Yunia Kadeghe Mbozi 16. Mrs. Karen Yunus Sengerema 17. Hassan E. Masala Kilombero 18. Bituni A. Msangi Nzega 19. Ephraem Mfingi Mmbaga Liwale 20. Antony J. Mtaka Mvomero 21. Herman Clement Kapufi Same 22. Magareth Esther Malenga Kyela 23. Chande Bakari Nalicho Tunduru 24. Fatuma H. Toufiq Manyoni 25. Seleman Liwowa Kilindi 26. Josephine R. Matiro Makete 27. Gerald J. Guninita Kilolo 28. Senyi S. Ngaga Mbinga 29. Mary Tesha Ukerewe 30. Rodrick Mpogolo Chato 31. Christopher Magala Newala 32. Paza T. Mwamlima Mpanda 33. Richard Mbeho Biharamulo 34. Jacqueline Liana Magu 35. Joshua Mirumbe Bunda 36. Constantine J. Kanyasu Ngara 37. Yahya E. Nawanda Iramba 38. Ulega H. Abadallah Kilwa 39. Paul Mzindakaya Busega (mpya) 40. Festo Kiswaga Nanyumbu 41. Wilman Kapenjama Ndile Mtwara 42. Joseph Joseph Mkirikiti Songea 43. Ponsiano Nyami Tandahimba 44. Elibariki Immanuel Kingu Kisarawe 45. Suleiman O. Kumchaya Tabora 46. Dkt. Charles O. F. Mlingwa Siha 47. Manju Msambya Ikungi (mpya) 48. Omar S. Kwaangw’ Kondoa 49. Venance M. Mwamoto Kibondo 50. Benson Mpesya Kahama 51. Daudi Felix Ntibenda Karatu 52. Ramadhani A. Maneno Kigoma 53. Sauda S. Mtondoo Rufiji 54. Gulamhusein Kifu Mbarali 55. Esterina Kilasi Wanging’ombe (mpya) 56. Subira Mgalu Muheza 57. Martha Umbula Kongwa 58. Rosemary Kirigini Meatu 59. Agness Hokororo Ruangwa 60. Regina Chonjo Nachingwea 61. Ahmed R. Kipozi Bagamoyo 62. Wilson Elisha Nkhambaku Kishapu 63. Amani K. Mwenegoha Bukombe 64. Hafsa M. Mtasiwa Pangani 65. Rosemary Staki Senyamule Ileje 66. Selemani Mzee Selemani Kwimba 67. Lt. Col. Ngemela E. Lubinga Mlele (mpya) 68. Iddi Kimanta Nkasi 69. Muhingo Rweyemamu Handeni 70. Lucy Mayenga Uyui MAJINA 63 WAKUU WA WILAYA WA ZAMANI NA VITUO VYAO VYA KAZI NA. JINA KITUO CHA KAZI 1. James K. O. Millya Longido 2. Mathew S. Sedoyeka Sumbawanga 3. Fatuma L. Kimario Igunga 4. Capt. (Mst.) James C. Yamungu Serengeti 5. Lt. (Mst.) Abdallah A. Kihato Maswa 6. Sarah Dumba Njombe 7. Jowika W. Kasunga Monduli 8. Elizabeth C. Mkwasa Bahi 9. Col. Issa E. Njiku Misenyi 10. John B. Henjewele Tarime 11. Elias W. Lali Ngorongoro 12. Raymond H. Mushi Ilala 13. Francis Miti Ulanga 14. Evarista N. Kalalu Mufindi 15. Mariam S. Lugaila Misungwi 16. Anna J. Magowa Urambo 17. Anatory K. Choya Mbulu 18. Fatma Salum Ally Chamwino 19. Deodatus L. Kinawiro Chunya 20. Ibrahim W. Marwa Nyang’hwale (mpya) 21. Dkt. Norman A. Sigalla Mbeya 22. Moshi M. Chang’a Mkalama (mpya) 23. Jordan M. Rugimbana Kinondoni 24. Georgina E. Bundala Itilima (mpya) 25. Halima M. Kihemba Kibaha 26. Manzie O. Mangochie Geita 27. Abdula S. Lutavi Namtumbo 28. Zipporah L. Pangani Bukoba 29. Dkt. Ibrahim H. Msengi Moshi 30. Col. Cosmas Kayombo Kakonko (mpya) 31. Lembris M. Kipuyo Muleba 32. Elinasi A. Pallangyo Rombo 33. Queen M. Mlozi Singida 34. Juma S. Madaha Ludewa 35. Angelina Mabula Butiama (mpya) 36. Hadija H. Nyembo Uvinza (mpya) 37. Ernest N. Kahindi Nyasa (mpya) 38. Peter T. Kiroya Simanjiro 39. John V. K. Mongella Arusha 40. Baraka M. Konisaga Nyamagana 41. Husna Mwilima Mbogwe (mpya) 42. Sophia E. Mjema Temeke 43. Francis Isaac Chemba (mpya) 44. Abihudi M. Saideya Momba (mpya) 45. Khalid J. Mandia Babati 46. Anna Rose Nyamubi Shinyanga 47. Dani B. Makanga Kasulu 48. Amina J. Masenza Ilemela 49. Mercy E. Silla Mkuranga 50. Christopher R. Kangoye Mpwapwa 51. Lt. Edward O. Lenga Kalambo (mpya) 52. Halima O. Dendego Tanga 53. Lephy B. Gembe Dodoma 54. Saidi A. Amanzi Morogoro 55. Jackson W. Msome Musoma 56. Elias C. B. Goroi Rorya 57. Lt. Col. Benedict Kitenga Kyerwa (mpya) 58. Erasto Sima Bariadi 59. Nurdin H. Babu Mafia 60. Khanifa M. Karamagi Gairo (mpya) 61. Gishuli M. Charles Buhigwe (mpya) 62. Saveli M. Maketta Kaliua (mpya) 63. Darry Rwegasira Karagwe

Wednesday, April 18, 2012

Wanakusini waazimia kuendeleza umoja kwa Maendeleo ya Lindi na Mtwara

Wadau wa kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara kupitia taasisi yao ya maendeleo ya kusini mashariki (SEDO) walikutana siku ya tarehe 15 Aprili 2012 mtoni kijichi, DSM nyumbani kwa mmoja wa wanakusini. Katika kikao hicho, wanakusini walirudia wito kwa kila mmoja kujitoa kwa hali na mali na kwa nafasi yake kuhakikisha maslahi ya wananchi wa kusini yanalindwa na kuzingatiwa.

Mambo mengi yalijadiliwa ikiwa ni pamoja na:
1. Kuimarisha nia ya ushirikiano kati ya wanakusini ili kuondoa udhaifu uliojengeka miaka nenda rudi ya utengano, kutopendana, kujijali binafsi na kutukuza marafiki wa nje ya Lindi na Mtwara kwa kupuuza undugu wetu;

2. kuhamasisha michango ya Fund raising iliyofanyika kwa mafanikio makubwa tarehe 18 Novemba 2011 pale Karimjee Hall, DSM ili fedha zikusanywe mapema na hivyo kufanikisha malengo yake;

3. Kutathmini kwa kina mikakati ya kuboresha sekta ya elimu kusini;

4. Kufuatilia uuzaji wa zao la korosho ambapo wananchi walio wengi na wanaotegemea korosho kama chanzo cha kipato chao cha mwaka hawajalipwa pesa zao na hivyo kuwafanya washindwe kumudu kujipatia mahitaji yao ya kila siku, kupeleka watoto shule na kujitibu pale wanapougua. Uongozi wa SEDO ulitoa taarifa ya ufuatiliaji huo ambapo uliarifiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya korosho kuwa makubaliano yameshafikiwa na vyama vya ushirika kuweza kupata dhamana ya serikali ili walipie tani karibu 85,000 zilizomo maghalani. Tayari tani zaidi 77,000 zilishanunuliwa na vyama hivyo vya ushirika.

5. Taarifa ya uongozi wa SEDO juu ya umaliziaji wa kilomita 60 za barabara ya kusini eneo la Ndundu - Somanga ambapo taarifa ni kuwa mkandarasi amelipwa pesa hivi karibuni na anafanya juhudi za kumalizia eneo lililobakia ambalo ni kama kilomita 40 hivi.

6. Wanakusini wameazimia kuwakumbusha wanachama wa SEDO na wanakusini wengine waweze kujumuika kwa pamoja, tuache utengano na kujiimarisha katika umoja ili kupitia SEDO mipango ya maendeleo ya kusini iwe na manufaa kwa ndugu zetu kule.

Kikao kijacho ni tarehe 06 Mei 2012, mahali pa kikao mtaarifiwa.

Imetolewa na:
SEDO Sekretariati
Dar es Salaam

Friday, April 13, 2012

Tandahimba Waandamana kushinikiza malipo ya korosho

MAELFU ya wakulima wa korosho wa Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara jana wameandamana kuishinikiza Serikali iwalipe malipo ya pili ya mauzo ya zao hilo, kama ilivyoelekezwa na Rais Jakaya Kikwete. Maandamano hayo yaliyoratibiwa na Chama cha Wananchi (CUF) wilayani humo, yalianzia ofisi za chama hicho saa 5:38 asubuhi na kuishia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo saa 6:10 mchana kabla ya kwenda kwenye mkutano. Maduka yalifungwa na shughuli zingine zilisimama kwa muda kuanzia asubuhi hadi baada ya maandamano na kusababisha watu kukosa huduma. Wakulima hao walibeba mabango yaliyo na ujumbe mbalimbali ambapo baadhi yalisomeka; “ahadi za kizushi tumechoka, ‘tulipe tusepe’… ‘fedha kwanza mazungumzo baadae ‘….’muda wa kusubiri umepita na agizo la Rais litekelezwe,” lilieleza bango hilo.
Kinyume na matarajio ya wengi, maandamano hayo ambayo yalitarajiwa kupokewa na Mkuu wa Wilaya, Hasna Mwilima yalikosa mpokeaji na hivyo kuwalazimu wakulima hao kukaa kwa karibu saa moja juani wakimsubiri Mkuu huyo wa Wilaya ili ayapokee.

Faragha zilitawala kwa viongozi wa CUF walioongozwa na Naibu Katibu Mkuu wake, Julius Mtatiro na hatimaye Mwilima alipokea maandamano hayo saa 6:59 mchana.

Akisoma risala ya wakulima hao, Katibu wa CUF wa Wilaya ya Tandahimba, Abasi Namanema alisema tangu kutolewa kwa tamko la Rais la kutaka wakulima hao walipwe malipo ya pili ya Sh 350 kwa kilo za korosho walizouza hakuna utekelezaji wa agizo hilo .


Mwilima alisema; “tatizo la korosho si la Tandahimba pekee, ni la mkoa mzima … kama mlikuja mkidhani kuwa DC atatangaza leo kuwa malipo ya pili yatalipwa lini mtakuwa mnanionea.”

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Michezo Tandahimba, Mtatiro alisema hawakuridhishwa na majibu ya Mwilima na kutafsiri kuwa kitendo hicho ni sawa na kutojua majukumu yake na hivyo hawana imani kama anaweza kuwa msaada katika hilo.

Chanzo: Gazeti la HabariLeo